Jumatano 19 Novemba 2025 - 22:28
Taarifa Muhimu Iliyo Tolewa na Vyama vya Lebanon: Mambo Sita Waliyoiomba Serikali

Hawza/ Vyama vya Lebanon vimetaka kuachiliwa kwa wafungwa wa Kilebanoni na Wapalestina ambao wako katika magerezani ya adui chini ya mateso mabaya kabisa, na vikasema kuwa suala lao ni sehemu isiyotenganishwa na mapambano.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kikao cha vyama, vikosi na watu mashuhuri wa kitaifa wa Lebanon kilifanyika Tripoli, Lebanon, katika makao ya Vikosi vya Nasseriyya, na baada ya kujadili masuala ya kitaifa na ya kimaisha, waliafikiana taarifa ifuatayo:

1. Mabadiliko ya msingi nchini Lebanon (kiuchumi na kisiasa)

Maisha nchini Lebanon kimsingi yamebadilika, si katika kiwango cha sarafu tu, bali katika muundo mzima wa kiuchumi na kisiasa. Kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kwa kiwango cha kutisha na kufikia mara mbili au tatu ya thamani yake kabla ya kuporomoka kwa uchumi si tukio la kifedha lililotengwa, bali ni matokeo ya moja kwa moja ya kugeuka kwa nguvu za kisiasa-kiuchumi kuwa mwakilishi wa ndani wa mfumo wa ulanguzi na unyonyaji.
Mshahara halisi umeshuka mno ikilinganishwa na uwezo wa awali, baada ya tabaka tawala kutumia mgogoro huo kugawa upya utajiri kwa manufaa ya benki chache, wafanyabiashara na wenye mitaji.

2. Utumiaji wa dola kama chombo cha uporaji

Bei kupanda kupindukia si hali ya vurugu isiyoeleweka, bali ni mfumo mpya uliowekwa na vyama vinavyotetea “udolareshaji” (Matumizi ya dola), na kuugeuza kuwa chombo cha uporaji uliohalalishwa. Udolareshaji haukurekebisha bei kama ilivyodaiwa, bali umeongeza gharama ya maisha, kutokana na sera zinazokusudia kuwafanya Walebanoni kuwa maskini na kugeuza riziki ya kila siku kuwa mapambano ya kuishi, imekuwa juu zaidi kuliko uwezo wa wanajamii.

3. Wasiwasi wa kifedha na Benki Kuu

Vyama vya Lebanon vinapinga jaribio la Benki Kuu kufunga taasisi ya “al-Qardh al-Hassan”; taasisi ambayo imeoyesha uadilifu, ukweli na uwajibikaji katika kurejesha dhamana za dhahabu kwa mujibu wa misingi yake, wakati benki za kibiashara zinaendelea kupora fedha za wateja bila uwajibikaji wowote.

Vyama hivyo vimeeleza pia wasiwasi wao juu ya mwelekeo wa kuongeza usimamizi juu ya uhamisho wa fedha kufuatia ziara ya ujumbe wa Wizara ya Hazina ya Marekani, na habari kuhusu kupunguzwa kiwango cha taarifa za miamala ya maduka ya kubadilisha fedha kutoka dola 10,000 hadi 1,000. Hili limegeuza usimamizi wa kifedha wa kigeni kuwa mzigo mpya kwa Walebanoni na kuzidisha udhaifu wa hali ya maisha.

4. Uvamizi wa Israel na kutofanya kazi kwa Kamati ya Usimamizi

Sambamba na kuporomoka huku, adui Mzayuni anaendeleza uvamizi wake unaoendelea kwa takribani mwaka mzima sasa. Utawala huu, kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na kupuuzia Kamati ya Usimamizi wa utekelezaji wake, umegeuza wajumbe wa kamati hiyo kuwa jukwaa la kutishia muqawama badala ya kumuwajibisha mkoloni.

Licha ya kamati hiyo—chini ya uongozi wa jenerali wa Kimarekani na wanachama kutoka Ufaransa, Lebanon, adui (Israel) na Unifilambayo iliundwa ili kudhibiti kusitishwa kwa mapigano iliyotangazwa tarehe 27 Novemba iliyopita, adui anaendelea na uharibifu, mabomu na mashambulizi ya angani kila siku, na anahifadhi vikosi vyake katika ardhi ya Lebanon kinyume na makubaliano.

5. Kubadilisha kanuni za mapambano na kulenga uwezo wa kuzuia uvamizi

Wakati hakuna uvunjifu wowote wa makubaliano uliorekodiwa kutoka kwa muqawama, maelfu ya uvunjifu umefanywa na Wazayuni, huku Kamati ya Usimamizi ikijihusisha na uchochezi dhidi ya muqawama na kudai kuporwa silaha zake.

Vyama hivyo vinaamini kwamba kinachoendelea mipakani kimezidi uvunjifu wa hapa na pale na kimegeuka kuwa juhudi za kubadilisha kanuni za mapigano na kulazimisha makubaliano mapya ya kiusalama yasiyo na uwiano. Lengo ni kulifanya azimio 1701 kuwa chombo cha kuishinikiza Lebanon, si adui, kwa ajili ya kutengeneza upya kanuni mpya zinazolenga uwezo wa Lebanon wa kuzuia uvamizi.

6. Maombi na mshikamano

Vyama hivyo vimeomba kuachiliwa kwa wafungwa wa Kilebanoni na Wapalestina walioko gerezani mwa adui chini ya mateso mabaya kabisa, na vikasema kwamba suala lao ni sehemu isiyotenganishwa na mapambano ya ukombozi wa kitaifa na kibinadamu.

Kikao cha vyama vya Lebanon kilihitimishwa kwa kutoa salamu na mshikamano kamili kwa wananchi wa Palestina huko Ghaza, Ukingo wa Magharibi na Palestina yote, huku kikisisitiza kuwa suala la Palestina litaendelea kuwa dira ya kitaifa, kijamii na kimataifa kwa mataifa na nguvu hai za eneo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha